Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

CHAGONJA AWAFARIJI ASKARI WALIOCHOMEWA NYUMBA MTWARA

$
0
0


Na Frank GeofrayJeshi la Polisi, Mtwara.


Kamishana wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja (pichani) amefika mkoani Mtwara na kuwafariji Askari wote waliochomewa nyumba zao na wahalifu wakati wa vurugu zilizotokea hivi karibuni wakati wa uwasilishaji wa bajati ya Wizara ya Nishati na Madini na kuwahakikishia kuwa Jeshi la Polisi litawakamata wale wote waliohusika katika vurugu hizo.
Vurugu hizo zilisababishwa na baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanapinga kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ambapo walifanya uharibifu wa miundominu mbalimbali ikiwemo kuchoma nyumba zaAskari Polisi.
Akizungumza katika kikao cha Maofisa na Askari polisi mkoani hapa Kamishna Chagonja alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema amesikitishishwa sana na vitendo vya uchomaji wa nyumba hizo na amewataka kutovunjika moyo katika kufanya kazi.
Alisema kilichowapata Askari hao ni changamoto katika kazi na wanapaswa kuzikabili ili kuhakikisha wanaendelea kulinda usalama wa raia na mali zao na raia wachache wasiopenda amani wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
“Raia wema ni wengi na wahalifu ni wachache hivyo lazima tuhakikishe wale wote wanaofadhili na kuhamasisha vurugu hapa mkoani mtwara tunawakamata na kuwafikisha mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa kuwa vitendo wanavyovifanya sio vizuri hasa kuchoma makazi ya watu”Alisema Chagonja.
Wakati huohuo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Ligula Dk Mohamed Kodi amesema katika kipindi chote cha vurugu zilizotokea mkoani hapa hakuna mgonjwa yeyote aliyefika hospittalini hapo na kulalamika kufanyiwa vitendo vya ubakaji kama taarifa zilivyoenea katika vyombo mbalimbali vya habari.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi Linus Sinzumwa alisema mpaka hivi sasa hawajapokea malalamiko yoyote kuhusiana na vitendo hivyo na amewataka kama wapo watu waliofanyiwa vitendo hivyo wapeleke malalamiko yao katika kamati iliyoundwa inayojumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
“Naomba malalamiko hayo yawe ya msingi na siyo ya uzushi na uongo na pindi ikigundulika kuwa maneno hayo ni ya uzushi na uongo sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wahusika” Alisema Sinzumwa.
Amewataka wakazi wa Mtwara kuendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili wahusika wote wa vurugu hizo waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>