Nimesoma hoja hii kwenye blog moja kwamba Adam Nditi mchezaji wa Chelsea yuko tayari kucheza national team lakini hajawahi kuitwa na kuna baadhi ya wapenzi wanatoa lawama nzito kwa chama cha Mpira na viongozi wandamizi wa TFF. Mimi kama muumini wa soka la bongo naomba nitaharishe chama cha mpira ili tusifanye yale ya zamani ya kumleta Kally Ongala huku tukijua ana uraia wa Uingereza na huku Tanzania sheria zetu zikiwa haziruhusu mtu kuwa na uraia wa Nchi mbili (Dual citizenship).
Adam Nditi yuko Uingereza toka akiwa mtoto mdogo kabisa hivyo sidhani kama kweli kijana huyu anaecheza Chelsea akawa anatumia passport ya Tanzania, ni na wasiwasi hatuna taarifa Za kutosha kuhusu huyu kijana. Ni kwasababu hiyo hatuwezi kukurupuka na kuwaandama viongozi wa TFF wakati hatujui status ya mchezaji mwenyewe.
Naomba kutoa hoja,
Onesmo Waziri