Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

makamu wa pili wa rais wa zanzibar ziarani pemba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa wakulima wa mashamba ya Mikarafuu kukubali kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa Kilimo hicho ili kujenga nguvu za uzalishaji wa uhakika wa zao Karafuu Nchini. 
 Balozi Seif alitoa sisitizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua baadhi ya Mashamba ya Serikali ya Miti ya Mikarafuu ambayo yako chini ya usimamizi wa baadhi ya wakulima ndani ya Mkoa wa Kusini Pemba. Alisema bado ipo dhana kwa baadhi ya wakulima wa Mikarafuu kujilimbikizia miti mingi ya zao hilo wakiwa na mawazo na fikra za kupata uzalishaji mkubwa zaidi jambo ambalo ni ndodo Kitaalamu. 
 Balozi Seif ambae amekuwa na utaratibu wa kutembelea mara kwa mara mashamba ya Mikarafuu hasa Kisiwani Pemba alieleza kwa kuwa Serikali Kuu inaendelea na Mikakati ya kuimarisha zao hilo Wananchi pamoja na Wakulima wa Kilimo hicho wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.
 “ Hivi sasa tunapaswa kuwa makini katika uzalishaji wa zao la Karafuu kitaalamu kwani wakati wa kuvuna karafuu mpeta umepitwa na wakati kulingana na mazingira yaliyopo ya soko la Dunia “ Alisisitiza Balozi Seif. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wakulima Abdulla Masoud Abdulla wa Kijiji cha Shungi na Mkulima Ali Othman Ali wa Kijiji cha Minazini kwa uamuzi wao wa kujikubalisha kuyahuisha mashamba ya Mikarafuu ya Serikali yaliyomo katika maeneo yao. 
 Balozi Seif alisema juhudi hizo zimeleta faraja kwa Serikali na kuwaahidi kwamba wao ndio wanaostahiki kupewa upendeleo wa kukodishwa wakati unapofikia msimu wa zao la karafuu. Naye Mkulima Ali Othman Ali wa Kijiji cha Minazini alimueleza Balozi Seif kwamba shamba hilo la Serikali lilikuwa pori tupu kwa muda mrefu na kulazimika kuliomba kulihuisha kutoka kwa Taasisi husika ili kulirejesha katika hali yake. 
 Mkulima Ali Othman alifahamisha kwamba alilazimika kutumia nguvu za ziada katika kulihuisha shamba hilo lenye ukubwa unaokadiriwa kufikia ukubwa wa Eka moja.
 Alisema hatua hiyo hivi sasa imempa faraja kwa vile tayari mazao ya Mihogo na Migomba aliyoiotesha ndani ya miti ya Mikarafuu iliyomo ndani ya shamba hilo imeanza kumpatia faida cha chakula sambamba na fedha za kujikimu kwa mambo mengine ya maisha. Naye Mkulima Abdulla Masoud Abdulla wa Kijiji cha Shungi amemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuzingatia ushauri wa wataalamu katika harakati za kuendesha kilimo hicho.  
Othman khamis Ame
 Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
 27/5/2013.
Shamba la Mikarafuu la Serikali lililo chini ya uangalizi wa Mkulima Ali Othman Ali wa Kijiji cha Minazini Wilaya ya Mkoani ambalo liko katika hali nzuri ya kupendeza baada ya kuhuishwa kwake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza Umuhimu wa Mashamba ya Mikarafuu kulimwa kwa Kitaalamu ili kukidhi mahitaji halisi ya soko la Kimataifa.
Mkamu Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia mazingira bora ya baadhi ya mashamba ya Serikali ambayo yamekuwa yakihuishwa na baadhi ya wakulima katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>