Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Tandika Bi. Rauva Maulid akieleza namna akina baba walivyo na tabia ya kuwarubuni mabinti wenye chini ya umri wa miaka 18 na kuwababishia Mimba,na kuongeza kuwa kwa tandika watoto wengi wanapata mimba wakiwa na miaka kuanzia miaka 12.
Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Said Mgeni akisisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa jirani na watoto wao ili waweze kuwa rafiki na kuwaeleza matatizo wanayoyapata kwa sababu kwa kufanya hivyo mabinti watakuwa huru kueleza matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la mimba.
Aisha mkazi wa Tandika akieleza namna vijana wanavyowarubuni na kuwasumbua ili waweze kushiriki nao katika ngono uzembe.
Kampeni ya Binti wa Kitaa huwakutanisha Mabinti pamoja na watu wa rika zote, hapa Msema chochote Steven Mfuko maarufu kwa Jina la Zero akiwa na Bibi Zakia Seif akiwafunda mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 kutokuwa na papara ya kukimbilia katika ngono.
Mmoja ya wageni waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa Jesca Kitomary alishauri kuwa wazazi wanatakiwa kuwaelimisha mabinti wao juu ya athari za mimba za utotoni na kuolewa mapema, kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata mimba na kuolewa kwa muda.