JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAJI |
TAARIFA KWA UMMA
Katika gazeti la Nipashe la Jumapili tarehe 12 Mei 2013 mwandishi Mashaka Mgeta aliandika makala yenye kichwa cha habari “Aibu kwa Profesa Maghembe na dharau kwa wataalamu wa Wizara” na kuwa, Wizara ya Maji imejiwekea rekodi chafu kwa bajeti yake kurejeshwa kabla ya kupitishwa na Bunge na wataalamuwa wa Wizara ya Maji wamekuwa miongoni mwa wasiosikilizwa na kupuuzwa suala hilo si la kweli.
Mnamo tarehe 24 na 25 Aprili, 2013, Waziri wa Maji Mhe. Prof. Jumanne Abdallah Maghembe (MB) aliwasilisha Bungeni Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2013/2014. Bajeti hiyo iliwasilishwa na mjadala uliendelea kwa muda wa Siku mbili.
jadala mkubwa ulikuwa Bungeni baada ya kuwasilisha maoni ya Kamati ya kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa Bajeti ya Wizara ya Maji haitoshi.
Mjadala ulihairishwa na Mhe. Spika chini ya Kanuni ya Bunge 67(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kama Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 2 Toleo la 2002.