Image may be NSFW. Clik here to view. ![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. John Baird alipowasili kwenye Hoteli ya HyattyRegency Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki Chakula cha Mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Membe. Mhe. Baird alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine pia walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Canada pamoja na kusaini Mkataba "Foreign Investment, Promotion and Protection Agreement" (FIPA). |
Image may be NSFW. Clik here to view. ![]() |
Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Baird wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu. |
Image may be NSFW. Clik here to view. ![]() |
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Baird akimsikiliza. Kushoto ni Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Alexandre Leveque. |
Image may be NSFW. Clik here to view. ![]() |
Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Baird zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. Picha na Rosemary Malale |