Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Jaji Sambo akimkaribisha Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania kuongea na Watumishi wa Mahakama ya Sumbawanga mapema leo Katika jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Jaji Mfawidhi Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo (aliyenyosha mkono) akimuelekeza baadhi ya maeneo Mhe. Jaji Mkuu na ujumbe wake alipotembelea jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe Jaji Mkuu yupo mkoani humo kwa lengo la kujionea Hali ya utoaji haki Katika Mkoa huo.
Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman ( wa nne kutoka kulia) akiwa Katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa alipotembelea Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mapema Leo, lengo likiwa ni kujionea hali ya utoaji haki Katika Mkoa huo.(Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).
Jaji mkuu Mohamed Chande aliyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya siku ya kwanza ya kukagua maendeleo ya utendaji haki kwa mahakam ya mikoa ya Rukwa na Katavi.
Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ni moja ya miundombinu za kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa uendeshaji wa kesi zao na pia kuondoa lawama za muda mrefu za uwajibikaji mdogo na vitendo vya rushwa.
Akiongea na watumishi wa mahakama hizo za hakimu mkazi wilaya na mkoa na baadae watumishi wa mahakama kuu kanda ya sumbawanga alidai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 10 zinategemewa ku[itishwa katika mwaka huu wa fedha wa utekelezaji mkakati.
Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Manase Goroba alisema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa ya wapiga chapa ikiwamo ya uchakavu wa majengo mengi ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa katika mahakama .
Alisema kuwa kumekuwepo na mahakama mpya ambazo ni zilijengwa kwa nguvu za wananchi na bado majengo hayo hajakamilika hivyo kunahitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo.
Mustafa sijani ni hakimu wa mwanzo wa wilaya walimweleza jaji mkuu kuwa adha zinazowakabili watumishi wa mahakama katika utendaji wa kazi ni pamoja na uhaba wa watumishi vitendea kazi.
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
Sumbawanga
JAJI mkuu wa Tanzania Mohamed Chande amesema kuwa mahakama kuu Tanzania inaendelea na mkakati endelevu wa miaka 2 utakao husisha unoreshajki wa miundombinu ya mahakama za ngazi zote nchini kutoa elimu ya kujiendeleza kwa watumishi wake na pia kuzitolea uamuzi kesi zote zilizochukua mda mrefu.