Washindi watatu wa promosheni ya shinda tiketi na Western Union wameondoka kwa shamra shamra Dar es Salaam juzi usiku kwenda kushuhudia fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Chelsea FC na SL Benfica iliyochezwa usiku wa kuamkia leo jijini Amsterdam.
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, mmoja wa washindi hao Bw. Quraish Shindo, amesema kwamba amefurahia sana nafasi aliyoipata kutoka kwa Western Union kwenda kuona mchezo huo laivu tofauti na pale alipokuwa amezoea kushuhudia kabumbu kwenye luninga.
“Unajua mi ni mshabiki mkubwa sana wa mpira wa miguu, kwahiyo nilivyoona promosheni hii, nikasema ngoja nijaribu bahati yangu. Mungu si Athumani, katika siku ya droo nikaibuka mmoja ya washindi na sasa niko hapa nikielekea Amsterdam kwa shauku kubwa,” Shindo alisema.
Aidha, Meneja Masoko wa Benki ya Posta (TPB) Bw. Andrew Chimazi amesema kwamba benki yao inaheshima kubwa sana katika kutoa huduma za Western Union na amefurahishwa sana na mshindi aliyepatikana kutoka benki kwake.
“Nawatakia safari njema washindi wote, pili napenda kuwahakikishia umma na watanzania kwamba bado promosheni hii inaendelea na zawadi mbali mbali bado zipo zakushindaniwa zikiwemo ving’amuzi kutoka Star Times,” Shimazi aliongeza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya Diamond Trust (DTB) Bi. Chandni Jiwa, alitoa rai kwa wateja mbali mbali wa benki hiyo kuendelea kutuma na kupokea fedha kupitia huduma yao ya Western Union ili waweze kujishindia zawadi zingine bwelele zilizobaki.
“Nawatakia safari njema na natumai washindi watafurahia fainali hiyo na mji wa Amsterdam Uholanzi kwa ujumla,” aliongeza Bi. Jiwa.
Washindi wengine wa Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyodhaminiwa na Western Union ni Flora Mbuya na Mzee Patropa Ndanshau.
Mbali na kutazama mechi, wakiwa jijini Amsterdam, washindi hao watatu watatembezwa katika vivutio mbali mbali vya utalii pamoja nakuhudhuria tafrija maalum ya ‘Western Union Experience’ itakayowakutanisha na washindi wengine kutoka nchi mbali mbali duniani. Washindi wa Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya wanatarijwa kurejea tarehe Mei 17, 2013, baada ya kushuhudia fainali hiyo kali baina ya timu ya Uingereza Chelsea FC na SL Benfica kutoka Ureno.
Kutoka kushoto katika picha ya pamoja ni Meneja Masoko wa Benki ya Posta (TPB) Bw. Andrew Chimazi, Quraish Shindo (mshindi), Flora Mbuya (mshindi), Mratibu wa promosheni hiyo kutoka 24D Brand Communications Bi. Farida Makame, Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya Diamond Trust (DTB) Bi. Chandni Jiwa na Bw. Patropa Ndanshau (mshindi) wakiwa uwanjani JNIA.
Mmoja wa washindi wa tiketi kuona fainali ya ligi ya mabingwa iliyodhaminiwa na Western Union Bw. Quraish Shindo akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu ushindi wake na safari ya kwenda kushuhudia fainali kati ya Chelsea FC na SL Benfica huko Amsterdam, Uholanzi
Meneja Masoko wa Benki ya Posta (TPB) Bw. Andrew Chimazi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma na promosheni za Western Union alipofika uwanja wa JNIA kuwatakia safari njema washindi.
Washindi wa Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) Flora Mbuya (kulia) na mwenzake Quraish Shindo wakiwa katika wakati wa furaha kabla ya kukwea kuelekea jijini Amsterdam kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Chelsea FC na SL Benfica
Safari ndo imeiva: Mzee Patropa Ndanshau, ambaye ni msanifu maarufu wa majengo (architect) wa kampuni ya Plan Associates ya Dar es salaam, akielekea katika mstari wa kukaguliwa uwanjani JNIA tayari kwa safari ya Amsterdam. Mzee Patropa alitabiria ushindi wa Chelsea FC dhidi ya SL Benfica.