Image may be NSFW. Clik here to view. ![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kitaifa. Katika Mkutano huo Mhe. Membe alifafanua juu ya hali ya kisiasa nchini Madagascar na Zimbabwe na kutoa taarifa za kuwasili kwa vikosi vya kulinda amani vya Tanzania huko Mashariki mwa DRC. Kuhusu masuala ya kitaifa Mhe. Membe alilitolea ufafanuzi suala la shambulio la bomu lilitokea hivi karibuni huko Arusha ambapo alisema kuwa Serikali inaendelea na uchunguzi na kwa ujumla hali nchini ni tulivu. Wengine katika picha ni Bw. John Haule (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe.Khalfan Juma Mpango (kulia), Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei, 2013. |
Image may be NSFW. Clik here to view. ![]() | ||||||||||||
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
|