Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

MADIWANI KILWA WAPITISHA MPANGO WA KUBORESHA MAENDELEO WILAYANI HUMO

$
0
0
Katibu Tawala msaidizi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Lindi,Abdul Dachi akitoa elimu kwa Madiwani ikiwemo wajibu na majukumu yao katika semina ya uelimishaji kwa madiwani ikiwemo kupitia mpango wa maendeleo ya wilaya hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Addoh Mapunda akitoa taarifa kwa Madiwani kuhusu Mpango wa Uboreshaji wa Wilaya ya Kilwa ikiwemo Upimaji wa Viwanja katika semina kwa Madiwani na kufuatiwa na kikao Maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kupitisha mpango wa maendeleo.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wakiwa katika kikao maalum ili kujadiliana na kupitisha mpango wa maendeleo ya wilaya hiyo.
Jumba la Maendeleo Wilayani kilwa jengo ambalo linatumika sasa katika kuendeshea vikao mbalimbali ikiwemo Baraza la Madiwani na hafla mbalimbali kama sherehe za Ndoa na burudani zingine na kupitia mpango huo Halmashauri itajenga ukumbi wa kisasa utakaogharimu tshs 3.5 Bilion.

Na Abdulaziz Video. 

Baraza la madiwani ktk halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, limepitisha kwa kauli moja Mpango wa kuboresha maendeleo ya halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa dhamana wa Taifa (UNIT TRUST OF TANZANIA}.

Mpango huo uliopitishwa, unajumuisha miradi miwili mikubwa ya upimaji wa zaidi ya viwanja 6,000 ktk mji mdogo wa Kilwa Masoko, mji mkongwe wa Kivinje na Nangurukuru pamoja na ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa Katika Mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Taarifa ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kilwa Adoh Mapunda kwa wajumbe wa Baraza hilo, imebainisha kuwa zoezi zima la utekelezaji wa mradi huo linategemewa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 8 ambapo shilingi bilioni 4.5 zitatumika kwenye upimaji wa viwanja na ujenzi wa ukumbi utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.5.

Akizungumzia juu ya tatizo sugu la upimaji wa viwanja katika halmashauri hiyo mkurugenzi huyo amesema kwa zaidi ya miaka 20 sasa kuna viwanja 200 tu vilivyopimwa na kuthibitishwa ktk mji wa Masoko na hivyo kusababisha upungufu mkubwa wa viwanja na kuwafanya baadhi ya watu kujenga kiholela au kulazimika kutoa rushwa kwa wafanyakazi wa idara ya ardhi ili kupimiwa viwanja.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>