Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha Yanga kesho kitaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumanne katika Mji wa Lubumbashi nchini Demokrasia ya Congo.
Mchezo huo utachezwa saa nane na nusu mchana kwa saa za Congo na unatarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka nchi tofauti wakiongozwa na mwamuzi wa kati kutoka nchini Angola.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini siku ya Jumapili kuelekea Lubumbashi Congo. kikiwa na wachezaji 21 pamoja na benchi la ufundi huku kesho hiyo majibu ya daktari yatatoka juu ya wachezaji majeruhi waliopo kwneye kikosi hicho cha wanajangwani.
Majeruhi ni Obrey Chirwa, Juma Abdul, Ally Mustapha 'batez', Geofrey mwashiuya, Nadir Haroub 'Canavaro' Juma Mahadhi aliyeumia katika mchezo wao dhidiya Azam wa Ngao ya Hisani na Kelvin Yondani.
Waamuzi wa mchezo huo ni Ref. Helder Martins De Carvalho(Angola), A.I Jean Claude Birumushashu(Burundi), A.II Arsenio Chadreque Marengula(Mozambique), R.R. Antonio Muachihuissa Caxala(Angola), M.C Gerges Rodolphe Bibi(Seylsius), R.A Ali Mohamed Ahmed(Somalia) na GC Russell Paul (Rep.of South Africa)
Yanga katika kundi lao wanashikilia mkia wakiwa na alama nne huku TP Mazembe akiongoza kwa kuwa na alama 10 akifuatiwa na ,edeama yenye alama nane na Mo Beajaia alama tano.