Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Dkt. Shein afanya uzinduzi wa barabara Mfenesini-Bumbwini Zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana,ujenzi huo umejenga na Kampuni ya Mecco kwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akizungumza na Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,wakikata utepe kufungua Barabara ya Mfenesini-Bumbwini,iliyojengwa na Kampuni ya Mecco kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ikiwa shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,(wa pili kulia) Naibu Waziri wa Mindombinu,Mawasiliano Issa Haji Gavu,(wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Miundombinu ,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma,(kushoto) wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini baada ya kufunguliwa Rasmi jana,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>