Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakuu wapya wa wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi kwa kujituma katika kuwatumikia wananchi na atakayeshindwa atamshauri Rais amtafutie wilaya nyingine.
Makonda ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha wakuu wa Wilaya Wanne kati ya watano katika jiji la Dar es Salaam, amesema Mkoa wake ni wenye idadi kubwa ya watu kuliko mikoa mingine hivyo kila mtu lazima afanye kazi ya kutatua changamoto zilizo mbele yake na bila kufanya hivyo nafasi ya ukuu wa mkoa itakuwa imemshinda.
Amesema kuwa wakuu wa wilaya wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni kupiga marufuku uvutaji wa shisha katika mkoa wa Dar es Salaam, Uvutaji Sigara hadharani na wataofanya hivyo watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Makonda amesema kuwa operesheni ya kuondoa ombaomba bodo inaendelea na wakuu wilaya wametakiwa kusimamia operesheni hiyo kutokana na mazingira mazuri ya elimu yaliyowekwa kwa watoto hao kusoma ili waweze kuachana na utegemezi huo.
Makonda amesema kuwa watu wanaowasaidia wanaomba wanafanya makosa kwa kufanya watu hao washindwe kuondoka katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha amesema kuwa tatizo la madawati bado lakini kuna upungufu wa vyumba vya madawati ambayo ni muhimu katika kuweza kuainisha katika kipindi hiki.
Wakuu wa Wilaya walioapishwa leo ni, Hashim Mgandilwa wa Kigamboni, Felix Lyaviva wa Temeke, Sophia Mjema wa Ilala na Ally Hapi wa Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya wa Ubungo Humphrey Polepole hajaapa kutokana na udhuru ya msiba wa baba yake mazazi ambaye ataapa baada ya kumaliza udhuru hiyo.
Wakuu wa Wilaya baada ya kuapishwa walikuwa na maoni tofauti, kwa upande Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Hashimu Mgandilwa amesema kuwa kazi yake ni kuitangaza Kigamboni kuwa ni Wilaya katika njia ya mbalimbali ya mawasiliano lakini sifa kwake kuanzisha Wilaya hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke amesema ametangaza kiama kwa ombaomba katika jiji na kutaka maafisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi yao na kama watashindwa atawashughulikia.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa amefanya kazi siku 74 kabla hajateuliwa na Rais ameweza kumaliza tatizo la madawati kwa Wilaya ya Kinondoni na kuahidi kuendelea na kasi yake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutumia wananchi katika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI