Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

CHUO CHA DIPLOAMSIA KUIMARISHA IDARA YA LUGHA ZA KIGENI CHUONI HAPO

$
0
0
Mshindi wa lugha ya kifaransa Eric Ngilangwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ushindi wake huo unaompa fursa ya kwenda nchini ufaransa kujifunza zaidi lugha hiyo, eric amepata fursa hiyo mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la uandishi wa insha kwa lugha ya kifaransa ,shindano liloandaliwa na ubalozi wa ufaransa nchini. kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia,Bw. Ismail Shah.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dr. Bernard Achiula akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) kuhusiana na juhudi mbalimbali ambazo chuo cha Diplomasia zinachukua katika kufundisha lugha za kigeni,katika hafla fupi ya kumpongeza mwanafunzi Eric kwa kufanya vizuri katika shindano ya uandishi wa insha ya kifaransa na kuibuka mshindi.Kulia kwake ni Mjumbe wa Bodi ya Chuo,Bw. Abdulrahman Abdallah.
Mshindi wa lugha ya kifaransa kutoka chuo cha Diplomasia bw Eric Ngilangwa(wa tano kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi, eric pia anachukua shahada ya post graduate katika chuo cha diplomasia.chuo cha diplomasia licha ya kutoa wataala wa utatuzi wa migogoro pia kinatoa kozi mbalimbali za lugha za kigen kama kifaransa, kireno, kiarabu,kihispania na hivi karibuni kichina kinaingia chuoni hapo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles