Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Watani wetu wa Jadi Wachemsha katika World Rugby Sevens Glasgow

$
0
0

Timu ya taifa ya mchezo wa Rugby nchini Kenya ilichemsha vibaya katika michuano ya Rugby sevens iliyofanyika katika uwanja wa Scotstoun, Glasgow siku ya jumamosi tarehe 4 Mei 2013. Walipoteza 17-14 Afrika ya Kusini katika mchezo wao wa kwanza na kufuatiwa kipigo cha 26-0 kutoka kwa Samoa katika mchezo wa pili. Mchezo wa tatu walishindwa kwa 10- 21 kwa Canada ambayo ilihafifisha matumaini yao ya kufanya kufanya vizuri katika Kombe Kuu la robo fainali katika siku ya pili.

Kutokana na kuchemsha kwao ni dhahiri kocha mkuu Mike Friday aliwapa wakati mgumu wachezaji baada ya matokeo mabaya yaliogubikwa na makosa makubwa ambayo yangeweza kwa urahisi kuepukwa. Kenya walionekana kana kwamba walipakwa grisi mikononi kabla ya mchezo kuanza na kufanya kuwa vigumu kupata mpira na kupoteza ki rahisi.

Ingawaje timu ya Kenya ilicheza vizuri kwa kiasi fulani katika mchezo wa kwanza, mchezo wao wa pili dhidi ya Samoa ulikuwa jicho-kidonda na kufanya mashabiki kuuma meno kutokana idadi ya makosa yaliyofanywa. Mchezo wao wa mwisho na Canada walijitahidi kurekebisha makosa yao ya awali na kutia bidii kukaba zaidi na kupunguza nafasi za kupokonywa mpira ingawaje waliishia kushindwa pia.

Kila wakati Kenya ilipokuwa na mpira, wao kuishia kufanya makosa, hivyo kupewa adhabu na penati. Mpaka sasa timu ya Kenya ina pointi 77 na kuwa na matumaini ya kufikia pointi 100 katika mwisho wa mzunguko. Hiyo ina maana Kenya inatakiwa na kuja na pointi 23 kutoka kwa timu ya Scotland na Uingereza. Kama wanaweza kuchukua pointi nane kwa kushinda Glasgow kisha wao kubakia na pointi 15 kwa kushinda Uingereza.

Afrika nzima inawakilishwa na Kenya pamoja na South Africa.
Canada wakijaribu kuizibiti Kenya kufunga goli.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>