Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh. Filiberto Sebregondi (katikati) akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya Wiki ya Umoja wa Ulaya itakayoadhimishwa nchini na kuhusisha shughuli mbalimbali za kijamii. Wengine katika picha ni Balozi wa Hispani nchini Mh. Luis Cuesta Civis(wa kwanza kushoto) , Balozi wa Ireland nchini Mh. Fionnula Gilsenan na ,Balozi wa Nethrland nchini Mh. Dkt. Ad Koekkoek Emmanuel .
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO_Dar es salaam
UMOJA wa Nchi za Ulaya (EU) umeahidi kuendelea kusaidia Tanzania katika miradi ya maendeleo, ambapo kwa mwaka ujao wa fedha wa 2013/2014 itaipatia Tanzania zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 562.
Kauli hiyo imetolewa leo na Balozi wa EU nchini Tanzania Mh. Filiberto Sebregondi jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya Wiki ya Umoja wa Ulaya itakayoadhimishwa nchini na kuhusisha shughuli mbalimbali za kijamii.