Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

MUHAS yaaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti

$
0
0

 Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo lililofungwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), Profesa Fredy Mhalu akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Washiriki Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kongamano hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 


=======  ======  ========

MUHAS yaaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti 


CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili (MUHAS) kimeaswa kuzidi kujenga uwezo wa ufanyaji tafiti mbali mbali zinazohusiana na masuala ya afya ili kuimarisha huduma ya afya nchini.

Akizungumza wakati wa sherehe za kufunga kongamano la Kwanza la Sayansi lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mganga Mkuu, Dk Donan Mmbando, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, alisema kuwa ili kuboresha huduma za afya nchini kuna haja ya watafiti na wataalamu kuendelea kutafuta njia za kuimarisha huduma hiyo licha ya changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta hiyo.

"Utaalamu katika kutafuta njia za kuboresha huduma za afya ni muhimu kwa watanzania wote. Nawasihi kuendelea kufanya tafiti lakini pia kuyatumia matokeo haya ya kitafiti kikamilifu ili kusaidia serikali kuboresha huduma ya afya kwa wananchi, "alisema Dk Mmbando.

Alibainisha kuwa ili kuboresha ,masuala ya afya wafanyakazi katika sekta hiyo wanahitaji kupewa mwanga zaidi kuhusiana na masuala ya afya na kupitia makongamano watapata elimu zaidi juu ya jinsi gani wanaweza boresha utoaji wa huduma za afya na kuleta ufanisi katika kazi yao.

"Tunahitaji kuendelea kukuza maarifa kwa kuendelea kuandaa makongamano ya aina hii zaidi hususani ya tafiti za masuala ya kisayansi na afya kwa kuwa yanatoa fursa za kubadilishana uzoefu na kutafuta mbinu mbali mbali za kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya afya.

"Makongamano ya kisayansi kama hili tunalofunga leo hii utoa fursa nzuri katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto nyingi za afya hususani jinsi gani ya kukabiliana na magonjwa kama malaria na vvu/ukimwi," aliongeza

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo hicho, Profesa Efata Kaaya aliipongeza serikali kwa kukiunga mkono chuo hicho hususani katika utoaji wa fedha ili kusaidia kufanikisha tafiti mbali mbali za kisayansi na kiafya zinazofanywa na chuo hicho nchini.

“Naishukuru serikali kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kipindi kirefu katika tafiti zetu hususani katika utoaji wa fedha ili kufanikisha tafiti hizi. Naimani kutokana na mchango huo, wataalam wetu wataendelea kutafuta mbinu jinsi ya kuboresha huduma za afya nchini,” alisema Profesa Kaaya.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>