Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

MSAADA TUTANI

$
0
0

Hii picha imenifanya nijiulize maswali mengi... wewe je? (ongeza kwenye comment)

1. Hayo maandishi yaliyoandikwa nyuma ya gari hilo ni wangapi wameweza kusoma? (OANGEZ, DANGEZ...)

2. Tanzania tunatumia lugha ya kiswahili zaidi, na kwenye gari hilo la mafuta hakuna neno lolote la kiswahili kumjulisha mtanzania kuwa hilo gari limebeba nini? na usalama wake ni nini?

3. Hapo inaonyesha hilo gari inamwaga mafuta kwenye tanki la chini la kituo cha mafuta katikati ya jiji la Dar es Salaam, na hakuna mhudumu yoyote aliyopo jirani nayo. je ikitokea bahati mbaya nani wa kulaumu?

4. Ndoo moja imelala chali jirani na kisima hicho... ilikuwa na nini? Maji/Mafuta/Mchanga...

5. Usalama wa gari na mali uko wapi?

6. Nijuavyo mimi, kila gari la mafuta inapewa sticker fulani ya kujulisha kuwa hilo gari limebeba mafuta ya aina gani, na kwenye ajali litazimwa na aina gani ya zima moto? kwenye gari hilo iko wapi?

7. Hiyo alama iliyoandikwa kulia la gari hilo (juu ya reflector) lina maana gani?

8. OSHA / EWURA / FAYA / N.K. ... mpo?

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>