Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

WANAFUNZI KUTOKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WANAOSOMA NCHINI ALGERIA WAKUTANA KUJADILI KUANZISHWA KWA CHAMA CHA EAC-STUDENTS IN ALGERIA.

$
0
0
Wanafunzi kutoka nchi 5 za Afrika Mashariki tunaosoma nchini Algeria tupo katika mchakato wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wanafunzi wote wa EAC wanaosoma katika nchi hii.Changamoto ya kuanzishwa kwa hii Jumuiya imetokana na idadi kubwa ya wanafunzi wa EAC wanaokuja kusoma kila mwaka nchini Algeria,Pia changamoto ilitokana na jitihada zinazo endelea sasa hivi nyumbani za ushirikiano wa nchi 5 za EAC.

Tukaona sisi kama Vijana kutoka EAC hili linatuhusu zaidi kwani sie ndo Taifa la kesho, na hivyo tukaona tuanzishe Jumuiya yetu hapa ili kuongeza ukaribu kati ya Vijana kutoka nchi 5 za EAC tukiwa hapa Algeria na baadae baada ya kumaliza masomo yetu.Pia hakuna nchi hata moja ya EAC yenye Ubalozi wake nchini Algeria na hivyo tunahitaji chombo cha kushughurikia matatizo yetu sisi sote kwa pamoja badala ya kuacha kila nchi kuwa kivyake na huku Serikali zetu zikitaka kuwa na Ushirikiano wa pamoja.

Kikao cha kwanza cha kujadili hili swala kilifanyika tarehe 03 mwezi Mei katika mji Mkuu wa Algeria, Algiers.Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi kutoka kila chama cha wanafunzi cha Nchi ya Afrika Mashariki ambazo ni Rwanda, Burundi,Kenya,Tanzania, na Uganda.Na wote tulikubaliana kuanzishwa kwa Jumuiya hii itakayo simama kwajina la EAC-Students in Algeria (EACSA).Changamoto tuliyonayo sasa nikupata baraka za Serikali zetu zote 5, pamoja na kusajili chama hapa Algeria.

Tunakuomba sana Kaka Michuzi kutumia blog yako ambayo hutembelewa sana na watanzania wengi waishio nje ya nchi kupata habari, kutangaza habari hii ili watu wote walioko hapa Algeria na sehemu zote wajue nini kinaendelea.

Na hiyo picha hapo ni picha ambayo tungepende iende sambamba na habari hii ni picha ya Viongozi wa Jumuiya za wanafunzi wa nchi za EAC, pamoja wadau wengine waliokutana kujadili swala hili.

Samahani sana kwa Usumbufu mkuu.

Wako katika kujenga Taifa,

Kikwembo D. Mlekwa,
Vice President EACSA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>