Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo
Na Ahmed mahmoud wa Globu ya Jamii, Arusha
MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja yu mahututi na wengine zaidi ya 49 wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka kitu kinachosadikiwa ni bomu majira ya saa 4 asubuhi leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.
Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisco Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat lebulu, na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.
Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .
Wengine ni Rioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo , ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.
Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
Umati wa wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo. Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.

Picha kwa hisani kubwa ya