Mama Ye! leo, Mei 5, inatoa wito kwa Mh. Dk Hussein Mwinyi (MB), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kushughulikia kwa haraka upungufu wa idadi ya wakunga wanaohitajika ili kuwasaidia akina mama wa Tanzania kujifungua salama.
Wakunga wana jukumu kubwa la kuwahudumia wanawake katika kipindi chote cha ujauzito na pia ni wataalamu wenye ujuzi wa kushughulikia matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua.
Wakunga wengi wanatembea umbali mrefu na kufanya kazi masaa mengi ili watoe huduma bora kwa wanawake katika jamii zao. Wataalamu wa masuala ya afya ya wajawazito na watoto wachanga wamekadiria kuwa, iwapo wanawake wote wa Tanzania wangepata huduma za wakunga wenye ujuzi, basi maisha ya akinamama wapatao 5,000 na vichanga 32,000 yangeweza kuokolewa ifikapo 2015.
Akiongea kwa niaba ya kampeni ya Mama Ye! Craig Ferla amesema: “Ni vyema kabisa kuwaenzi wakunga wetu katika Siku ya Wakunga Duniani. Tunapongeza ahadi za serikali kuitilia mkazo sera ya huduma za afya ya uzazi kuwa bure, lakini mengi bado yanahitaji kufanyika ili kuongeza idadi ya wahudumu wa afya.”
Takwimu zilizochapishwa na ripoti ya Hali ya Wakunga Ulimwenguni (State of the World’s Midwives) zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji wakunga 9,941 zaidi ili kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 la kuwa na asilimia 95% ya wajawazito wanaozalishwa na wahudumu wenye taaluma.
Craig Ferla ameongeza kuwa: “Tunawaalika na kuwahimiza Watanzania kutoa shukrani kwa wakunga – na kusaidia kuwapa moyo vijana nao waamue kuwa wakunga siku za baadae. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia ‘Twitter’ ukiwaambia asante kwa kujituma kazini, pia waweza kuweka picha kwenye ukurasa wetu wa ‘Facebook’ zinzazowaunga mkono wakunga wetu wa Tanzania pamoja na mathalan kutambua juhudi kubwa za mkunga unayemthamini kwa kazi zake kubwa katika jamii yako.”
Ukitaka kufahamu zaidi kuhusiana na hali ya wakunga nchini Tanzania, tembelea tovuti ya www.mamaye.or.tz/sw ambapo utapata ushahidi uliowekwa kwa namna rahisi kuelewa, habari kuhusu mashujaa katika uzazi salama, ahadi zilizowekwa na serikali na hatua mbali mbali unazoweza kuchukua web: www.mamaye.or.tztwitter: @MamaYeTZfacebook: facebook.com/MamaYeTZ
MamaYe! 164C Msasani Beach, Kinondoni, P.O. Box 13731, Dar es Salaam, Tanzania Phone: +255 (0) 754 588 233 ili kufanikisha kampeni hii muhimu. Ipaze sauti yako isikike na toa madai ya msingi zaidi, jiunge na kampeni ya Mama Ye!