Dun and Bradstreet Credit Bureau, Ofisi ya kwanza yenye kibali cha kutunza kumbukumbu za Mikopo Tanzania, Dar es Salaam imepanga kukutana na kushauriana na watendaji wakuu wa Benki zote Tanzania katika semina iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt-Kilimanjaro siku ya tarehe 3/05/2013.
Uwepo wa Dun and Bradstreet Credit Bureau nchini Tanzania unategemewa kwa kiwango kikubwa kuimarisha na kujenga daraja kati ya Benki ya Tanzania na Sekta za Benki.
Warsha hii inaambatana na utambulisho na ufunguzi wa ofisi ya Dun&Bradstreet Credit Bureau nchini Tanzania, semina hii inalenga kukuza mahusiano kati ya ofisi hii, mabenki na taasisi zote za kifedha ambazo zimeleta mchango muhimu katika kuhakikisha kwamba wanapata ofisi ya kudhibiti kumbukumbu za mikopo yenye viwango vya kimataifa.
Kwa mujibu wa Bwn. Miguel Llenas – Mkurugenzi Mkuu wa Dun & Bradstreet Credit “Lengo kuu ni kujenga taasisi itakayoweza kusimamia jukumu la kuinua uchumi wa Tanzania na utimamu katika taasisi za fedha na Benki. Kwa maana hii, semina hii itaeleza kwa kina jinsi ya kusaidia benki na taasisi za fedha nchini Tanzania juu ya kutathimini na kuboresha maombi ya mikopo/mkopo kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanakuwa na habari na utambuzi juu ya waombaji wa mikopo katika mabenki na taasisi zao.”
Pia, katika semina hii, meneja mkuu wa Dun & Bradstreet Credit Bureau - Adebowale Atobatele amesema “Tumeangazia mabenki na taasisi za fedha nchini Tanzania kuwa washirika wetu. Fursa pekee ya kukutana, kusikilizana na kushauriana na washirika wetu katika hili semina. Tunahitaji kuwatumikia wao na ni muhimu kuelewa changamoto husika wanazokumbana nazo katika biashara hii ya ukopeshaji. Tunaamini ufumbuzi wa kuendeleza maslahi bora ya mabenki, sekta za fedha na uchumi watanzania, na watanzania kiujumla ni kwa kupata michango mbalimbali kutoka katika benki na taasisi za fedha ambazo zitakutanisha taarifa za mikopo zitakazotambuliwa katika kiwango cha kimataifa”.
Kwa muda mrefu, mabenki na taasisi za fedha nchini Tanzania zimekuwa zikiweka kumbukumbu juu ya uwiano wa mikopo isiyofanya vizuri katika vitabu vyao kiasi inafikia kiwango cha kusamehe madeni hayo na kurekodi faida ndogo. Uanzilishi wa taasisi ya kutunza kumbukumbu za mikopo katika mifumo ya kibenki, taasisi za kifedha na wateja, itasaidia kuleta mwangaza katika siku zijazo.
Semina iliyoandaliwa na Dun & Bradstreet Credit Bureau inafuatiwa na mafanikio ya shughuli zake katika ofisi zilizopo Ghana ambapo soko lake limekuwa kubwa kwa uwepo wa D&B nchini Ghana.
Soma zaidi kuhusu D&B hapa www.dnbcb.com
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dun & Brandstreet Credit Bureau Adebowale Atobatele akiongea wakati wa semina ya maofisa wa benki na taasis za fedha uliofanyika Dar es Salaam May 3 2013. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Miguel Llenas.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Miguel Llenas akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam 03 May 2013 wakati wa semina ya wa semina ya maofisa wa benki na taasis za fedha. Kushoto ni kuhusu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Adebowale Atobatele.