Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

KUTOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMII

$
0
0
Ankal akiwa na Dkt Licky Abdallah na mtangazaji Chacha Maginga wa TVT (siku hizi TBC1) wakati wa uchambuzi wa mechi za Kombe la Ulaya (UEFA Championship) kwenye stesheni hiyo mwaka 2004 zilizofanyika Ureno (Portugal).
Euro 2004, kama ilivyojulikana, ilikuwa michuano ya 12 kwa timu za Taifa za soka za wanaume za Ulaya zilishindana, na kwa mara ya kwanza ilifanyika Ureno toka Juni 12 hadi Julai 4 katika miji minane tofauti ya Aveiro, Braga, Coimbra, Guimarães, Faro/Loulé, Leiria, Lisbon na Porto.

Jumla ya timu 16 ilishiriki katika michuano hiyo iliyoshuhudia Ujerumani, Spain na Italy wakiondolewa katika hatua za makundi, ambapo bingwa mtetezi, Ufaransa, aliondolewa na Ugiriki katika robo fainali,na wenyeji Ureno wakazinduka baada ya kufungwa kwenye mchezo wa ufunguzi na kufika fainali, kwa kuwafunga Uingereza na Netherlands.
Mwaka huo kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa fainali ikizikutanisha timu zilizofungua dimba (wenyeji Ureno na Ugiriki), ambapo Uguriki walishinda na kushangaza wengi kwani waliwahi kufuzu mara mbili tu katika michuano mikubwa – Euro 1980 na kombe la dunia mwaka 1994. Na ushindi wao katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ureno ulikuwa wa kwanza katika michezo yote ya fainali waliyowahi kucheza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles