Mnara wa Askari jijini Dar es salaam enzi hizi na hizi sasa.
Hii ni kumbukumbu ya askari jeshi waliopigana katika vita ya kwanza ya dunia inayosimama kuangalia bandari ya jiji hilo.
Ilizinduliwa mwaka 1927. Sanamu hiyo ya askari wa British Carrier Corps iliundwa Uingereza na mchonga sanamu Mwingrereza aitwaye James Alexander Stevenson ambaye katika sanamu hii katumia jina lake la kufikirika la “Myrander”.
Kabla ya kupelekwa Dar es salaam sanamu hii ya Askairi ilioneshwa kwa muda jijini London katka Royal Academy. Kabla ya kuwekwa sanamu ya askari, mahali hapa palikuwa na sanamu ya Meja Herman von Wissman, gavana wa wakati huo wa German East Africa, iliyozinduliwa mwaka 1911. Waingereza walipoingia Dar es salaam mwaka 1916, waliibomoa sanamu ya gavana wa Kijerumani pamoja na zingine za Karl Peter na Otto vo Bismarck zilizokuwa hapo. Sanamu ya askari ya Dar es salaam ni moja kati ya tatu zilizozinduliwa wakati mmoja kati ya tatu zilizoweka katika mwaka huo wa 1927 sehemu za koloni ya Uingereza ya Afrika Mashariki (British East Africa). Zingine mbili zilikuwa Mombada na Nairobi.