Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KFC-Tanzania,Bwa.Simon Schaffer akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa tawi lao lilipopo Mikocheni karibia na shule ya Feza jijini Dar,Tanzania.Bwa.Simon alisema kuwa wazo la kufungua mgahawa huo nchini Tanzania,ni wazo ambalo limechukua muda wa miaka 3 kutimiza,amesema kuwa KFC itahakikisha viambata vinavyotumika kuandaa vyakula vinapatikana kutoka kwa wasambazaji waliokidhi vigezo vya viwango na ubora,aidha alibainisha kuwa Wafanyakazi wa mgahawa huo (ambao kwa asilimia kubwa ni Watanzania),walipata mafundisho ya miezi 6 kwa malengo ya kuboresha uwezo wao katika kuhudumia wateja kwenye sekta ya vyakula.
"Nasubiri sana kwa hamu kuona jinsi Watanzania watakavyo furahia chakula na huduma za KFC,huduma zetu zimeandaliwa kwa kuzingatia jinsi ya kuwapa wateja huduma kwa haraka na ubora,tunafurahia sana kwa kuanza kuhudumia soko la Tanzania na kuleta huduma tofauti na iliyo bora zaidi",alisema Bwa.Simon.KFC ina migahawa zaidi ya 17,000 duniani historia yake ikianzia huko Kentuky nchini Marekani.
Mmoja wa Wafanyakazi wa mgahawa wa KFC,Faraja Kilongole akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani), namna walivyopata mafunzo jinsi ya kuwahudumia wateja kupitia mgahawa huo,ambao ndio mara ya kwanza kufunguliwa nchini Tanzania.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgahawa wa KFC,wakishangilia jambo mara baada kuzinduliwa rasmi na kuanza kuwa tayari kuanza kuwahudumia wateja mbalimbali watakaokuwa wakiwasili kwenye mgahawa huo.