DR. FRANCIS MW. MSELLEMU
Baba, ni miaka 17 sasa tangu ulipotuacha!
Haijawahi kuwa rahisi kwetu, kwani kila iitwapo leo machungu na majonzi yetu ni kama jana.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia nafasi ya kuwa na Baba kama wewe, na nafasi ya kuishi nawe kwani kwetu ulikuwa Rafiki na Mwalimu.
Kwa Mapenzi ya Mwenyezi Mungu, tunaendelea kukua kiimani tukiamini kwamba ipo siku moja tutakutana nawe tena.
Pumzika kwa Amani Baba!