Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 10 YA FAO LA ELIMU LA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (Watatu kulia), Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Gaudentia Kabaka (Wanne Kulia), Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (Wakwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Profesa Adolf Mkenda (Wapili Kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Wakwanza kulia), wakiimba wimbo wa taifa mwanzoni mwa sherehe za miaka 10 ya fao la elimu litolewalo na Mfuko huo. Sherehe hiyo ilifanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye sherehe iliyofanyika juzi kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akipokea zawadi toka kwa naibu waziri wa fedha, Saada Mkuya Salum kwa niaba ya PPF kwenye sherehe za miaka 10 ya Fao la Elimu litolewalo na Mfuko huo kwa watoto ambao wazazi wao walikuwa wanachama wa Mfuko huo kabla ya kufariki. Sherehe hizo zilifanyika Jumamosi iliyopita kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akimkabidhi zawadi ya laptop, mwanafunzi Baraka Jacob, ambaye alipata daraja la kwanza kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012. Baraka ni mmoja kati ya wanafunzi 1,333 waliofaidika na fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, kutokana na kufariki kwa wazazi wao ambao walikuwa wanachama wa Mfuko huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (Katikati), Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira), Gaudentia Kabaka (Wakwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPF, Profesa Adolf Mkenda (Kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto na walezi wao ambao wanafaidika na fao la elimu litolewalo na Mfuko huo.
Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Gaudentia Kabaka (Kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Wiliam Erio, wakifurahia jambo wakati wa sherehe hizo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiwatuza wasanii wa taarab wa kikundi cha “Isha Mashauzi” waliotumbuiza kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, pamoja na wakurugenzi wa Mfuko huo, wakiwa kwenye sherehe hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>