Hawa ndio watu watatu kati ya wanne wanaoonekana katika picha ya hpo chini. walibeba vibuyu vyenye udongo wa Tanganyika na Zanzibar na Chungu kilichotumika na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuchanganyia udongo huo ambapo mara baada ya zoezi hilo ndipo jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi miaka 49 iliyopita. Kutoka kushoto ni Mama Sifaeli Chuma aliyebeba kibuyu chenye mchanga wa Tanganyika, akifuatiwa na Bw. Omar Hassan Mzee aliyebeba chungu kikubwa na Bi Khadija Rajabu Abbas aliyebeba kibuyu chenye udongo wa Zanzibar.
↧