MTOTO SAMWEL MLOPE
Unaweza kujiuliza ni nini ambacho kimetokeza katika mgongo wa mtoto huyu?.Mtoto Samwel Mlope mwenye umri wa miaka kumi na moja(11) ambaye ni mkazi wa Mahenge ndani ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Mtoto huyu alianza kuumwa mwaka 2001 ambapo alianza kusumbuliwa na tatizo la moyo kuwa na tundu.
Kwa mara ya kwanza kabisa alipoanza kusumbuliwa na tatizo hili mama yake mzazi ambaye ni Bi. Amina Ally alimpeleka katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na baadae akaambiwa ampeleke mtoto huyo katika hospital ya Taifa Muhimbili na baada ya kufika muhumbili ndipo alipoambiwa kuwa mtoto Samwel anasumbuliwa na tatizo la kuwa na tundu kwenye moyo wake.
Afya ya mtoto Samwel wala hairidhishi kabisa,hali iliyompelekea kushidwa kabisa hata kupata masomo.
Na huyu ndiye mama mzazi wa mtoto Samwel Mrope,Bi. Amina Ally ambaye anajishughulisha na kazi za ndani ili aweze kujipatia pesa kwa ajili ya kujikimu kimaisha yeye pamoja na mwanae samwel. Alisema kuwa "baba wa mtoto Samwel aliondoka muda mrefu sana uliopita kuelekea machimbo kwa ajili ya kutafuta na mpaka hii leo hajarudi na hawafahamu yupo wapi.
Bi. Amina alisema kuwa "ninawaomba watanzania wote kwa ujumla waweze kunisaidia ili mwanangu Samwel aweze kupelekwa nchini India na kupata matibabu kwani mwanangu anapata shida sana"na hatimaye aliweza kuzitoa namba zake za simu kwa watu ambao watajitokeza kutoa msaada kwa mtoto Samwel ambazo ni 0752 732290.