NduguWaTanzania,
Kwa Niaba ya TAWI la Chama Cha Mapinduzi Uingereza ,na kwa niaba yangu binafsi, Napenda kutoa salamu za dhati kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein, kwa Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania,na kwa WaTanzania wote kwa ujumla kwa kutimiza miaka 49 ya Muungano wa nchi yetu, TANZANIA.
Pamoja na salamu hizo, binafsi na kwaniaba ya wana CCM UK ,napenda kuwaomba na kuwakumbusha WaTanzania wenzangu, tuendelee kuuenzi na kuulinda Muungano wetu kwa kudumisha AMANI, UPENDO, UMOJA, UTULIVU na MSHIKAMANO. Hizi ndizo silaha zilizoweza kuulinda Muungano huu ambao umetuletea Heshima ya kipekee Duniani kote, kwa takriban nusu karne sasa.
Ndugu WaTanzania, nawasihi kamwe tusichezee amani tuliyonayo. Tujifunze kutoka nch mbalimbali duniani ambazo wamechezea amani yao na sasa wamo ndani ya dimbwi kubwa la machafuko, mauaji ya halaiki na yanayoendelea kila kukicha. Maelfu ya raia wasio na hatia wamepoteza maisha yao katika Nchi mbalimbali, wengine kupata ulemavu wa kudumu, kupoteza makazi na kuharibikiwa na mwenendo mzima wa mfumo wa maisha yao, milipuko ya mabomu isiyoisha na raia kukosa amani na utulivu. WaTanzania kamwe tusikubali kuipoteza amani yetu kwa uchochezi wa watu wachache, na ambao kwa sababu zao binafsi hawatutakii mema , na mpaka wako tayari kutumia visingizio kama vya siasa na dini ili watusambaratishe.
Aidha, WaTanzania wa Nje ya Nchi (Diaspora)tunajivunia na kutambua kwamba tuna nafasi ya pekee ya kuchangia katika maendeleo ya Nchi yetu Tanzania katika Nyanja tofauti . Mojawapo ya Mchango wetu Mkubwa kwa Taifa ni kufuatilia kwa ukaribu mambo yanayoendelea nyumbani ,nakutoa mchango wetu wa kimawazo pale inapobidi.
CCM-UK tutaendelea kutoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhur iya Muunganowa Tanzania Dr.JakayaMrishoKikwete , pamoja na Serikali yake anayoiongoza kwa kuona umuhimu wa kutushirikisha WanaDiaspora na kuthamini mchango wetu.Tunafarijika sana na kuahidi siku zote kwamba tutaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania, kama inavyowezekana kwa raia wengine
Weng Ulimwenguni wanaoishi nje ya Nchi zao na wanachangia kukuza uchumi na kuendeleza jamii zao kwa kutumia ujuzi na ufanisi waliojifunza ughaibuni.
MWISHO WaTanzania wenzangu, tusherehekee sikukuu ya Muungano wetu kwa Amani na Utulivu, tuvumiliane na sote tutie nia ya kudumisha na kuulinda Muungano wetu na kuwapuuza wale wote wasioutakia wema Muungano wetu.
Tuwaenzi waasisi wetu Baba waTaifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuulinda Muungano, kudumisha amani na utulivu, aidha kufanya kazi kwa juhudi na kuinua uchumi wa nchi yetu hadi kufikia azma ya - MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, SI NDOTO YANAWEZEKANA.
Kwa Niabaya CCM UK – Nawatakia WaTanzania wote popote pale walipo Dunian iMaadhimisho na Sherehe njema za siku hii adhimu.
MUNGU IBARIKI AFRIKA - MUNGU IBARIKI TANZANIA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
-----------------------------------------------------
Mariam A. Mungula
KATIBU
CHAMA CHA MAPINDUZI – UINGEREZA
IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI – CCM-UK