Rai imetolewa kwa Watanzania kuwa na matumizi sahihi ya fedha wanazopata kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashindano ya michezo ya kubahatisha ili kuweza kujiletea maendeleo na kuondoka katika wingu la umasikini, Rai hiyo imetolewa na mmoja ya washindi wa promosheni ya Vodacom MAHELA Bi. Catherine Gumbo mkazi wa Pugu Kajiungeni - Jijini Dar es Salaam inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake Pugu Bi. Catherine amesema kuwa ushindi wa shilingi milioni tano kwake umekuja muda muafaka huku wakati akiwa amekwama kuendelea na shughuli za ujenzi kwa miaka kadhaa. Bi Catherine ametanabaisha kuwa ni vyema sasa watanzania wakawa na mipango na matumizi sahihi ya fedha wanazoshinda kwani ni fedha ambazo zinakuja wakati mtu hajategemea.
"Ushindi wa milioni tano kwangu umekuwa ni faida kubwa, hadi sasa nimefanikiwa kumalizia sehemu kubwa ya ujenzi wa nyumba yangu ambao ulikwama kwa muda mrefu, nimenunua madirisha ya aluminium (9)na nyavu zake ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 2 kama mnavyoona, nikanunua vigae vya ndani na kutengeneza mfumo wa maji ndani ya nyumba na niko katika hatua za mwisho kuvuta umeme kama ambavyo mmeshuhudia mpembuzi kutoka Tanesco akiwa hapa, alifafanua Bi. Catherine na kuongeza kuwa, " Ni vyema sasa Watanzania tukawa na matumizi sahihi ya fedha ambazo wanashinda kutokana na Promosheni hizi zinazoendeshwa na makampuni mbalimbali hapa nchini,kwani ni fedha ambazo zinakuja wakati mtu hujatarajia, Pia ni vyema hata kampuni ambazo zinaendesha promosheni hizi kuweka mipango maalum ya elimu kwa wateja au hata mafunzo ya ujasiliamali au kilimo kwa washindi wanaokuwa wanapatikana ili fedha hizo ziwe na manufaa kwa watanzania, alihitimisha Bi Catherine.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw. Matina Nkurlu, amesema kuwa hakika watu aina ya mama Catherine ni mfano wa kuigwa miongoni mwa watanzania kutokana na mafanikio ambayo ameyapata hadi sasa.
"Vodacom tunajivunia sana mafanikio ya mama Catherine, kwa maendeleo ambayo ameyafanya kwa kiasi kidogo alichokipata ni dhahiri kuwa promosheni hii imekuwa na mafanikio na kubadili maisha ya Watanzania," alisema Nkurlu.
Hadi sasa washindi zaidi ya 332 wamepatikana huku 26 wakijinyakulia milioni 5 na wengine 249 wakijinyakulia milioni 1 kila mmoja na kufikisha Shilingi Milioni 380 zilizotolewa hadi sasa huku milioni 100 zikiwa zimesalia kufikia tamati ya promosheni hiyo tarehe 29 ya Mwezi huu ambapo mshindi wa jumla ataibuka na fedha taslimu shilingi milioni 100.
Bi Catherine Gumbo (49 ) Mkazi wa Pugu - kajiungeni Dar es Salaam, akimuonyesha Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw. Matina Nkurlu Sehemu ya nyumba ambayo anaendelea kuijenga kutokana na fedha za Ushindi alizopata kupitia promosheni ya Mahela inayoendeshwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania. Vodacom ilimtembelea Cathrine nyumbani kwake jijini dar es salaam kuona jinsi fedha za ushindi zilivyosaidia kuboresha maisha yake.
Mama Mzazi wa Mshindi wa promosheni ya Mahela, Bi.Grace Gumbo akimuonyesha Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni ya Vodacom Bw.Matina Nkurlu, Jumla ya pointi alizojikusanyia hadi sasa kutokana na ushiriki wake katika promosheni hiyo inayoendelea kwa wateja wa Vodacom nchi nzima. Kushoto ni Catherine Gumbo aliyejishindia Sh 5 Milioni, Vodacom ilimtembelea Cathrine nyumbani kwake jijini dar es salaam kuona jinni fedha za ushindi zilivyosaidia kuboresha maisha yake.