Wakazi wa Kimanzichana wakifurahi wakati mbunge wao alipokuwa akiulizwa maswali ya kumuudhi na na kusababisha kuzungumza kwa ukali kwenye mkutano huo. |
KATIKA hali isiyo ya kawaida mkazi mmoja wa kijiji cha Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Rajabu Juma Mkumba, amesema wananchi wa kijiji hicho wameacha kuwapeleka shule watoto wao na badalayake wanawapeleka madrasa kutokana na gharama za madrassa hizo kuwa za bei ya chini kuliko Shule.
Akimuuliza swali mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Adam Malima, alisema wanashangazwa na kitendo wanachofanyiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimanzichana Kusini cha kuwalipisha ada ya Shilingi Ishirini Elfu kwa motto mmoja anaetaka kuanza darasa la kwanza.
“Mheshimiwa mbunge Mkuu huyu wa shule anatoa wapi sharia ya kutuchangisha shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kila mwanafunzi anaeanza darasa la kwanza? Wakazi wa hapa wengi wanaona bora watotowao wawapeleke madrassa kule kwasababu adayake ni ndogo,” Alihoji Mkumba.
Lakini katika hali ya kushangaza mbunge huyo aligeuka mbogo na kuanza kuwafokea wananchi hao na kuwaambia hayo wamejitakia wenyewe kutokana na kutofanya juhudi ya kujenga shule nyingine kwani alishawaambia miaka miwili iliyopita kuwa watafute kiwanja ili ijengwe shule kwakua wao wanaongezeka sana.
“Nakumbuka miaka miwili iliyopita niliwaambia kwenye mkutano hapahapa kwamba kasi yetu ya kuongezeka ni kubwa mno hivyo tujitahidi kutafuta kiwanja mapema ili tuwe na shule nyingine lakini hadi leohakuna kilichofanyika,” Alisema Malima.
Aidha mbunge huyo aliwaambia wananchi hao kama wanania ya kweli ya kutaka kutatua baadhi ya matatizo yao inawabidi wafanye ushirikiano wa dhati kwani wenzao wa kijiji Cha Mwalusembe walishirikiana nay eye wakaweza kujenga madarasa manne kwa siku 45 lakini kijiji hicho kinamiaka miwili hakijajenga hata darasa moja.
Mkutano huo ulikuwa ni wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii kwa wananchi kwenye Wilaya hiyo, ambapo wananchi wengi walionekana kuwa na maswali mengi yaliyokuwa nnje ya mada na maudhui ya mkutano huo hali iliyopandisha hasira za mbunge huyo na kuahidi atakwenda tena tarehe 17 mwezi huu kukutananao.