Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

watuhumiwa 19 wa fujo za liwale mkoani lindi jana wahojiwa na polisi

$
0
0
Mnamo tarehe 23 April, 2013 majira ya saa tisa alasiri, huko wilayani Liwale mkoani Lindi, kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wakulima wa Korosho walijaribu kuzuia gari lililokuwa na malipo ya korosho wakipinga malipo ya pili ya Korosho na kuanza kufanya vurugu na uhalibifu mkubwa wa mali, ambapo mpaka sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa nyumba kumi na nne (14) zimechomwa moto, baadhi ya mifugo imejeruhiwa na kuangamizwa na kufanyika uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema ametuma timu maalum ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCP Issaya Mngulu kwenda kuongeza nguvu mkoani humo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa katika kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inarejea haraka na wale wote waliohusika kufanya vitendo vya uhalifu wanakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, mpaka sasa jumla ya watuhumiwa kumi na tisa (19) wamekamatwa kwa mahojiano.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini linalaani vikali vitendo hivyo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi na badala yake kuwataka wananchi kufuata njia ya kufanya majadiliano pale ambapo kutakuwa na migogoro ya aina yoyote ndani ya jamii. Majadiliano yatasaidia kuepusha madhara yanayojitokeza ikiwemo watu kupoteza maisha, uhalibifu wa mali na misongamano ya wahalifu magerezani.

Wakati hatua hizo za kisheria zinaendelea kuchukuliwa, Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa watulivu na waendelee kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini wahalifu hao wachache wanaochochea vitendo vya vurugu na kufanya uhalibifu wa mali ili hatiamae waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Taarifa zaidi juu ya tukio hili zitaendelea kutolewa na uongozi wa mkoa wa Lindi baada ya tathmini ya uharibifu uliofanyika kukamilika.

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (TZ).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>