Baadhi watu waliokuwemo kwenye mashua hiyo wakijaribu kutafuta uelekeo mara baada ya mashua hiyo kuanza kuzama kwa sababu ambazo bado hazijajulikana. Bahati njema baadae abiria wote waliokolewa na boti. Ajali hiyo imetokea leo jioni maeneo ya Kisiwa cha Chumbe, kati ya Dar es salaam na Unguja ambako Globu ya Jamii ilipita na kukutana na ajali hii ambayo hadi tunaruka hewani hakukuwa na habari ya mtu aliyepoteza maisha.
Baadhi ya abiria katika mashua hiyo wakiokolewa baada ya mashua yao kupoteza muelekeo. Kwa habari zaidi tuvute subira kidogo. Tutawaletea taarifa kamili itakapopatikana