Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Washiriki wa Kitanzania wa Programu ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Waanzisha Tawi Tanzania

$
0
0
 African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi Ijumaa jioni katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt
 Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda  ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt
 Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii , ambayo nae alikabidhiwa na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi
                                         Mwenyekiti wa AWEP Tanzania, Bi Flotea Masawe.
              Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt,  ambao ni wafadhili  wa AWEP  katika mkakati wake wa kuwakwamua wanawake  wajasiriamali wa Afrika
                    Waziri Abdallah Kigoda akiwasili katika hafla ilofanyika jioni hii, na kuhudhuriwa na wanachama kutoka sehemu mbalimbali nchini, ambao baadhi walikuwa katika mafunzo ya kujifunza ujasiri amali ambao unalengo la kuwafanya wawekezaji
Mama Lowasa pamoja na Balozi Maajar walihudhuria uzinduzi huu wa AWEP Tanzania
Baadhi ya wanachama wa AWEP Tanzania Chapter katika picha ya pamoja na mgeni rasmi sambamba na Balozi Alfonso
burudani ilikuwa toka kwa Makumbusho Traditional Dancers
Picha na Shamim Zeze


Wajasiriamali wanawake wa Kitanzania waliowahi kushiriki katika Programu ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wameanzisha tawi la Tanzania la Chama cha Wajasiriamali Wanawake wa Afrika (AWEP). Tawi hilo limezinduliwa leo katika hoteli ya Doubletree, Hilton jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na Balozi wa Marekani Alfonso E. Lenhardt na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda.

Katika hotuba yake wakati wa hafla hii, Balozi Lenhardt alisema, "Kuzinduliwa kwa tawi la Tanzania la AWEP kunaanzisha rasilimali muhimu kwa wajasiriamali wanawake nchini kote. Hivi sasa wanawake wajasiriamali nchini Tanzania watakuwa na chombo watakachoweza kukitumia kubadilishana mawazo na uzoefu wao kuhusu mbinu bora za kuanzisha na kuendesha biashara. Balozi Lenhardt alisisitiza kuwa " Tawi la Tanzania la AWEP ni kielelezo cha dhamira na jitihada za wanawake wa Tanzania za kuwajengea uwezo wanawake wenzao nchini. Tawi hili litakuwa ni mtandao mwingine wa kukuza sekta binafsi nchini na kuwasaidia wajasiriamali wanawake kutimiza ndoto zao."

AWEP ilianzishwa mwaka 2012 na  washiriki wa Programu ya kila mwaka ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kama hatua ya kwanza ya mkakati wa kujenga mtandao wa wajasiriamali wanawake kutoka nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara waliodhamiria kubadilisha jamii zao kwa kumiliki na kuendesha biashara ndogo ndogo na za kati na kuwa sauti ya kuchagiza mabadiliko ya kijamii katika jamii hizo.

Msemaji wa Ubalozi wa Marekani Bi. Dana Banks alisema, " Hadi mwishoni mwa mwaka huu ambapo awamu ya tatu ya ziara za mafunzo nchini Marekani itakapokuwa imekamilika, jumla ya wanawake wajasiriamali 122 wanaojihusisha na biashara ndogo na za kati katika kilimo, usindikaji vyakula, mavazi, ubunifu, mapambo ya nyumbani na sekta nyinginezo watakuwa wamehudhuria program ya AWEP."

AWEP ni programu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inayolenga kuinua usawa wa kijinsia kwa kuongeza ushiriki wa wanawake wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Aidha, programu hii inalenga kujenga mtandao wa wajasiriamali wanawake  katika nchi hizo waliodhamiria kuchangia kuleta mabadiliko ya kijamii, ukuaji uchumi na kupanua ukubwa na wigo wa biashara kikanda na kimataifa, hususan kuongeza biashara na Marekani kupitia mpago wa AGOA.

Mwenyekiti wa tawi la Tanzania la AWEP Bi. Flotea Massawe alisema "tawi hili litajenga mwamko wa wanawake wa Kitanzania na kuwawezesha kubadilishana uzoefu wao. Aidha, litawapatia nyenzo na fursa za kuwa viongozi katika jamii zao kwa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jamii zao na kuwawezesha kuwa sauti ya mabadiliko."



Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>