Jeneza la marehemu Bob Sambeke likiwa nje tayari kwa ajili ya kuuaga mwili
Juu na chini ni Mtoto wa marehemu Jamal akifungua jeneza la marehemu baba yake Bob
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho
Watoto wa marehemu Sia na Getrude
Baadhi ya waombolezaji waliofika msibani hapo
Watu wakibadilishana mawazo kwa huzuni
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi kuzika
Gari liliokuwa limebeba mwili wa marehemu Bob
Baadhi ya waombolezaji na magari eneo la tukio nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha
Umati mkubwa wa watu ulifurika nyumbani kwa marehemu “Babu Sambeke” eneo la njiro jijini Arusha kuuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi .
Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka Arusha na Moshi wakionekana kutawala msiba huo.
Magari ya kifahari nayo yalitawala na kusababisha msongamano mkubwa kwenye barabara ya Njiro.
Shughuli hizo zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalum la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwa ajili ya maziko.
Katika zoezi hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu .
Ndani ya jeneza marehemu alivishwa nguo zake za urubani.
Tofauti na ilivyozoeleka katika misiba mingine hapa nchini, katika msiba huu watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia wenyewe, vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi kinywaji hicho.
Marehemu ameacha watoto watatu ambao ni Sia, Jamal na Getruda.