Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115310

HOJA YA HAJA YA MBUNGE WA KILWA KASKAZINI KUHUSU GESI ASILIA

$
0
0

Sekta ya gesi na mafuta ni moja kati ya sekta kubwa na ngeni kwa kiasi fulani hapa nchini.
Kwa kipindi cha miaka mingi na haswa miaka ya sabini na themanini Serikali ya awamu ya kwanza ilifanya kazi kubwa ya uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesi nchini  lakini bila ya mafanikio ya uwekezaji.
Hii inaweza kuwa ilichangiwa sana na siasa zilizokuwapo kwa wakati ule kwa maana ya umagharibi na umashariki na pengine imani ya wawekezaji kutokana na msimamo tuliokuwa nao kama nchi  katika suala la ukombozi wa bara la afrika dhidi ya ukoloni pia uduni wa hali ya teknologia ya wakati ule na ukweli kwamba eneo letu la nchi za mashariki mwa Afrika ilijulikana kuwa ni ukanda wa gesi asilia tu  na enzi zile gesi asilia ilikuwa haina thamani kuliko mafuta.
Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni , nchi yetu imefanikiwa sana kuwavuta wawekezaji katika sekta na nyanja tofauti  sana ikiwamo katika gesi na utafiti wa mafuta. Hii ni nafasi nzuri tuliyoikosa kwa miaka mingi kiasi cha kutuweka nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingi za afrika na dunia ya tatu.
Lakini sasa kiasi kikubwa tumeanza kuona manufaa ya uwekezaji ule japo kwa uchache na changamoto nyingi ndani yake.
Tumeanza mwaka 2012 na kumaliza na mfululizo wa matukio ya aina tofauti kwa waandishi kuandika makala na habari nyingi kuhusu shughuli na sekta nzima ya gesi nchini ,na mara ya mwisho kabisa kufuatia maandamano ya wanachi wa Mtwara ambao walitokea katika vyama  tofauti.
Sikuona tatizo la waandamanaji wale pamoja na ujumbe ulitolewa bali baadhi ya ujumbe  unaonyesha zipo tafsiri nyingi zaidi ya madai ya mahitajio ya manufaa ya mapato katika uwekezaji wa gesi na bomba la gesi.
Nilipata wasisiwasi mkubwa sana baada ya kuona wanaojua ukweli wa jinsi mambo yalivyo na wale wasiojua kuamua kwa dhati kabisa kuupotosha umma wa watanzania  na dunia kwa ujumla.

Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini na mjumbe wa POAC



Viewing all articles
Browse latest Browse all 115310

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>