Katika kuendelea kuboresha mahusiano bora kati ya Benki na wateja wake, Tawi la Benki ya CRDB Meru liliandaa siku maalum kwa ajili ya watoto iliyoitwa Junior Jumbo Day.
Siku hiyo ilikua ni kwa ajili ya kuwakutanisha wazazi, watoto na wafanyakazi wa Benki katika mazingira tofauti na ya kiofisi ambapo michezo mbalimbali iliandaliwa kwa ajili ya watoto huku pia zawadi mbalimbali zikitolewa kwa watoto.
Pamoja na hayo vyakula na vinywaji mbalimbali viliandaliwa kwa ajili ya watoto na wazazi/walezi wao. Yafuatayo ni baadhi ya matukio ya picha zilizochukuliwa kwenye tukio hilo.
Afisa masoko wa Benki ya CRDB akihudumia watoto waliofika katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha kwenye siku maalumu ya Junir Jumbo Day.
Watoto wakifurahia michezo mbalimbali ya iliyoandaliwa katika siku maalumu ya watoto (Junior Jumbo Day ) katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
Watoto wa shule za msingi Hady,Kilimani,St Patrick,Green Acres na watoto wa wateja wakisherehekea siku maalum ya watoto iliyoandaliwa na Benki ya CRDB,tawi la Meru kwa ajili ya watoto iliyofanyika tarehe 6/06/2013 jijini Arusha katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
Watoto wakishindana kwenye mchezo wa kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
Mmoja ya watoto walioshinda moja ya michezo iliyoandaliwa na kukabidhiwa zawadi na Meneja wa tawil la Meru Bi. Loyce Kapaliswa katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
Watoto wakijiandaa kushindana mchezo wa kukimbia na magunia katika viwanja vya Olasiva Park Garden.