Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni eneo kubwa la savana na misitu Kaskazini mwa Tanzania ikitapakaa katika mikoa ya Mara na Arusha. Eneo lake ni kilomita za mraba 14,763 na kijiografia inaendelea kidogo ndani ya Kenya katika Hifadhi ya Masai Mara.
Katika hiifadhi ya Serengeti kuna idadi kuba ya wanyama pori. Serengeti inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, twiga , kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya wanadamu wa kale kabisa yalipatikana liko ndani ya Serengeti. Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia iko katika kaskazini-magharibi ya Tanzania na inaenea kwa kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki.
Ina eneo la mraba kilometa 30,000 2. Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi dunian, na hua ni tukio la nusu mwaka. Uhamiaji huu ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu.
Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai, yaani "Serengit" kumaanisha "mbuga isiyoisha". Mnamo mwezi wa Oktoba, karibu herbivores (yaani wanyama wanaokula majani badala ya nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua.
Katika mwezi wa Aprili, wanyama hao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena huvuka Mto wa Mara. Jambo hili kwa mara huitwa "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu takriban 250,000 hufa safarini wakati wa uhamiaji huu.
Vifo hivyo mara nyingi husababishwa na kuliwa na wanyama wakali ama uchovu. Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.Kwa mnaopenda utalii wa ndani si vibaya mkapanga kutembelea hifadhi ya Serengeti
Tembo wakiwa Serengeti
Simba wakila pozi
Swala
Hawa hawana mchezo na mtu...
Pundamilia