Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli. akiongea leo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo lilikoporomoka ghorofa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo, akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka.
Kamati hiyo imeziamuru halmashauri za Wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni kufanya tathmini ya majengo yote na kuchukua hatua mara moja zitapogundulika zimejengwa chini ya kiwango.
Tayari watu 11 wanaotuhumiwa kuhusika katika ujenzi wa ghorofa lililoporomoka wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kuua bila kukusudia

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka akiwa eneo la jengo lilioporomoka. Nyuma yake ni jengo ambalo linajengwa na mjenzi yule yule aliyejenga liliporomoka. Kamati hiyo imetoa siku nne kwa mjenzi kubomoa jengo hilo ambalo linasemekana nalo limejengwa chini ya kiwango.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk TerezyaHuvisa wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka na Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli akijadili jambo na Bw. Azim Dewji pamoja na mjumbe wa kamati Mhe Zakhia Meghji. Picha na mdau Sujit Bhojak