Heri ya mwaka mpya 2013 watanzania wenzangu ,tunauanza mwa huu mpya kwa msimamo mmoja wa kukuza maendeleo ya michezo na sanaa nchini kwetu Tanzania,
Watanzania tuna uwezo mwingi wa kufanya mambo makubwa katika medani za kimataifa, kama vile muziki ,michezo na mambo mbalimbali, ila hatuna ushirikiano ,vilevile pia kudharauliana kwingi, kitu anchofanya mzawa watu hukibeza na kikidharau badala ya kukisapoti. Hivi nani anajua kama kuna Mtanzania toka Zanzibar alikuja Marekani akiwa na umri wa miaka 15 anaitwa FRED MERCRYhttps://www.youtube.com/watch? v=xdCrZfTkG1c&feature=youtube_ gdata_player,mwanamuziki ambaye nyimbo zake mpaka leo hii zinatumika katika michezo mikubwa kama vile Baskett ,football hockey na mingeneyo hapa nchini Marekani katika utangulizi kabla ya mchezo kuanza
Sio huyo tu tuna watu mbali mbali toka nchini ambao wameonyesha vipaji nje ya nchi kama akina Filbert Bayi ,John Bura, Nyambui katika mbio Rashid Matumla ngumi, mpira Peter Tino ,Dilunga , MOGELLA Pondamalli na wengineo walitufikisha katika fainali za kombe la Afrika miaka ya 80 mwingine mwanzilishi wa Bongo flavaDandu muziki wake unapigwa nje mpaka leo.Sasa kwanini tuishie hapo wakati uwezo tunao, ila ni sababu hatuna ushirikiano.Hatuthamini vitu vya nyumbani tumeupa nafasi utamaduni wa kigeni badala wa nyumbani.
Mfano mzuri mimi ni mwafrika wa kwanza ambaye nguo zangu zinavaliwa Dunia nzima , lakini watanzania wenzangu badala ya kuniunga mkono ndio kwanza wanabeza na kudharau nguo, gani hizo kisa Kajumulo katengeneza. Sasa sio wakati wa kuilaumu serikali eti haitusaidii badala ya kujilaumu wenyewe kwa roho zetu za ubinafsi.
Tunasema serikali imetutelekeza vijana, huku tukitaka wazee wote wang'atuke kwenye uongozi je? ni kweli unafikiri tutafika kwa mtindo huu wa vijana kuinga tamaduni za kigeni si tutashia Tanzania kuwa Taifa la kigeni. hivi inakuwaje wasanii vijana wa nyumbani tunashindwa hata kuuzaata hata nakala 200 tu za CD nje ya nchi Wakati huo tunatumia pesa za kigeni kununulia vifaa hivyo vya muziki wakati vinatupotezea hela haviingizi kutoka nje.
Ushauri wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo na sanaa nchini kwetu Tanzania, nchi yetu haiwezi kuendelea kimichezo na utamaduni bila ya kuwa na ushirikiano mkubwa baina yetu.Huwezi kumuona Mwingereza kavaa jezi ya Simba ama Yanga au kuona Mwamerika anasikiiza muziki wa Diamond lakini nyumbani kila kijana anatamani awe mwamerika .je vijana mna haki ya kulalamika serikali umewatupa?
Siongei hivi kama mwanasiasa ila nina uchungu na maendeleo ya nchi yangu .Nipo huku ugenini kwa ajili ya maslahi ya nchi yangu,sijaiba wala kufanya biashara haramu, ninachotaka ni kuonyesha kwamba kumbe kuna watanzania ambao wanaweza kufanya biashara nje ya nchi na wakakubalika.
Hizo ni salamu zangu kwa mwaka huu 2013 tupige harambee ya michezo na sanaa ili mataifa mengine yatujue ,mpaka sasa nimeshauza zaidi ya milioni 20 nguo za kajumulo lakini ni watanzania wachache wanaunga mkono je Addidas, Nike , Puma na Kappa wasingesaidia nchi zao kimichezo wangefika wapi ?
HIVYO NAOMBA USHIRIKIANO...
HERI YA MWAKA MPYA
ALEX KAJUMULO