Kamishna wa Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kulia) akiongea jambo na Clemence Tesha ambaye ni mjumbe wa kamati ya sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Emmanuel Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania akichangia mada kuhusu utendaji kazi wa maafisa ugavi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Juma Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi Tanzania akielezea jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia taaluma ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Mkurugenzi wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma.
Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea kuhusu umuhimu wa kuboresha rasimu ya Sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu hiyo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. Kulia ni Dk. Godfrey Sansa kutoka Chuo hicho.
Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma.Picha na Anna Nkinda – Maelezo