Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Dc Kilwa aagiza watendaji kutoa huduma kwa jamii kwa Muda Muafaka

$
0
0

Na Abdulaziz,Lindi
MKUU wa wilaya Kilwa Mkoani Lindi Mhe Abdallah Ulega (pichani juu)  ameeleza  kuwa wakati umefika sasa kwa watendaji na viongozi wa umma  kufanya kazi ya kuwahudumia  wananchi  bila ya kuwapangia muda maalumu wa kuonana nao. Aliyasema hayo katika  ziara mbalimbali za kukagua miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali za Wilaya hiyo .

Mhe Ulega akiongea na baadhi ya watendaji amewaasa kuacha urasimu wa utoaji  wa huduma kwa  jamii  na kubainisha kuwa Watendaji na watoa huduma mbalimbali za jamii kuwa vikwazo hali inayochangia wananchi kukosa imani na serikali yao kutokana na  vitendo/taratibu za kuwahudumia wananchi  ikiwemo kuwapangia muda maalumu wa kuonana nao kupata huduma stahiki  hali ambayo ni moja ya vikwazo vinavyolalamikiwa sana Wilayani Humo .

‘Mtumishi wa umma ni Yule aliyetayari kuwahudumia wananchi  kwa misingi ya haki, unyenyekevu nidhamu na uadilifu asiyekuwa tayari kufanya hivyo aamue kuacha kazi na kabla ya watu  kuichukia  na kuisema vibaya serikali yao wale wote watakao fanya kazi kwa  mazoea na kutotenda haki  kwa katika kutoa huduma kwa wakati wawajibike kabla hawajawajibishwa kwa sababu Hatuwezi kukubali kuona serikali ikitukanwa  na kupakwa matope kwa uzembe na makosa ya mtendaji  mmoja ambaye hataki kuwajibika”  alisema Ulega.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mhe Addo Mapunda (picha ndogo) akiongea na Globu ya Jamii  alibainisha kuwa ofisi yake imejipanga kuhakikisha Jamii zinapata huduma stahiki zinazotolewa na Halmashauri hiyo na kuahidi kueleza kuwa kipo kitengo cha kupokea Kero na Malalamiko ili kutafutiwa ufumbuzi.

 ‘Mwandishi nakuhakikishia Maagizo ya Mkuu wa Wilaya kuhusu watendaji ninayashughulikia ipasavyo na ndio maana naalika watendaji wa kata wote na maafisa Tarafa wote kila kukiwa na Baraza la Madiwani ili nao wafikishe ujumbe kwa wananchi wao maazimio  yote yanayotolewa na kupitishwa na Madiwani’

Aidha Mapunda alisisitiza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha Elimu inayotolewa wilayani humo Inaboreka ili kuondoka na aibu ya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho na kutoa wito kwa jamii kushirikiana vema na Walimu waliopangwa katika shule zao ikiwa pamoja na kuanza kujenga nyumba bora kusaidia watumishi wanaoletwa kwa Kushirikiana ili walimu hao wafurahie kuishi


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>