Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere akipongeza uzinduzi huo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere baada ya kutoa hotuba ya uzinduzi wa mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa mkoa wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
Sehemu ya magari matano ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu la Arusha.