Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa Kusaidia Jamii - Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni. Fedha hizo zimetolewa kumalizia ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba.
Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa Kusaidia Jamii - Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akikabdhi kwa mmoja wa wazee wa shehia ya Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni. Fedha hizo zimetolewa kumalizia ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha Michenzani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika eneo hilo. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa(wa pili kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakishudia.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa akielezea ukwa Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalim(mwenye fulana nyekundu) ujenzi wa jengo jipya la kituo cha Afya cha Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba muda mfupi kabla ya Vodacom Foundation kukabidhi hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa akiongoza kikundi cha ngoma ya kibati kutoka Chokochoko Mkoa wa Kusini Pemba kucheza ngoma hiyo wakati wa haflka ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni kumalizia ujenzi wa kituo cha Afya cha Michenzani Kisiwani humo zilizotolewa na Mfuko wa Vodacom wa kusaidia Jamii - Vodacom Foundation. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule akifurahia burudani hiyo.