Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 121831

WAKANDARASI WAASWA KULINDA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI-OSHA

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha sheria wa Wakala wa usalama na afya mahali pa kazi(OSHA),Joyce  Mwalubungu, akizungumza na wakandalasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mshauri mkuu wa ufundi wa ujasiliamali na miradi kwa vijana Jelous Chirove akizungumza na wakandarasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkaguzi mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano katika jengo la Kazi House jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakandarasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)



Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

 MAKANDARASI wametakiwa  kuwajibika kwa kuwahudumia wafanyakazi wao wakiwa sehemu ya kazi kwa kulinda afya na usalama  wakiwa kazini.
Hayo yamesemwa  na Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Usalama na afya  Mahala Pakazi (OSHA),Akwilina Kayumba wakati wa Warsha ya Wakandarasi iliyoandaliwa  na Wakala wa Usalama na Afya sehemu ya kazi  uliofanyika leo katika Ukumbi wa Shirika la Kazi Duniani, jijini Dar es salaam.

Warsha kwa hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa Makandarasi  katika kuelekea kuadhimisha siku ya usalama na Afya Mahala Pakazi  Duniani ya afya  Duniani itakayofanyika Aprili 28 mkoani Dodoma.
Amesema sekta ya ujenzi ina wafanyakazi wengi hivyo inatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu katika kuepuka ajali ambazo zinaweza kutokea wakiwa kazini pamoja na magonjwa.

Kayumba amesema katika maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahala Pakazi Duniani,Wakala usalama na afya Mahala Pakazi kwa maadhimisho hayo itakuwa  siku ya maombolezo,majeruhi,magonjwa na vifo vya wafanyakazi mahala  pakazi.

Amesema kauali mbiu ya maadhimisho ya siku usalama na Afya Mahala Pakazi  Duniani mwaka huu ikiwa na kauli mbiu ‘Tushirikiane sote kudumisha usalama na afya sehemu ya kazi’.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 121831

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>