Kijana Zuberi Mgeni anayesumbuliwa na maradhi ya moyo yanayopelekea tumbo kujaa maji, anahitaji kiasi cha dola 6000 sawa na shilingi 9.6 milioni kwa ajili ya kwenda India kufanyiwa upasuaji wa maradhi yanayomsumbua.
Mjomba wa Zuberi, twaha yusuf ugama anasema kulingana na majibu ya madaktari Zuberi anatakiwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya tatizo lake ikiwa ni pamoja na oparesheni ya kubadili valve za moyo.
"Vipimo vilifanyika mwezi January, tuliambiwa tuandike barua ya kuomba msaada lakini tangu hapo hatujajibiwa, hivyo tunawaomba wasamaria wema wamchangie kijana huyu ili aweze kufanyiwa upasuaji kuokoa maisha yake.
Zuberi mwenye umri wa miaka 18 anasema maradhi hayo yamemsababishia maumivu yanayoambata na tumbo kuvimba kupita kiasi pamoja na miguu yake kuvimba ,kushindwa kupumua vizur,kua na mchoko uliopitiliza, hali inayomsababishia karaha na maumivu aliyoyavumilia kwa miaka mitatu sasa.
"Napumua kwa shida, siwezi kutembea pia ninapata shida wakati wa kulala maisha yangu yamebadilika na wala sina tegemeo kwa maisha yajayo," ni maneno ya kijana Zuberi Mgeni anayesumbuliwa na tatizo la kuvimba kwa tumbo na miguu.
Hali hiyo imepelekea afya ya kijana huyo kudhorota na tumbo kuwa na ukubwa wa zaidi ya mama mjamzito wa miezi 9, miguu yake kuvimba huku sehemu nyingine za mwili zikionyesha kudhoofu.Inakadiriwa kiasi cha lita za 15 zimerundikana mwilini kwake.
Akizungumza na Mwananchi juu ya maradhi hayo Zuberi anasema mnamo mwaka 2006 akiwa darasa la tatu katika shule ya Kwale Kizingani Mkoani Tanga, tumbo lake lilivimba kupita kiasi alipelekwa hospitalini na kupewa dawa zilizomrudisha katika hali yake ya kawaida.
"Ilikuwa likizo, nilikula chakula mchana kwa kuwa sikujisikia vizuri, nilikuwa na homa kali iliyoambatana na mafua nilikwenda kupumzika, nilipoamka jioni saa 12 tumbo langu lilikuwa limevimba sana, nilikwenda hospitali ya Kizingani na kupatiwa dawa, hapo ndipo lilitoweka. Niliendelea na shule hadi mwaka 2010 nilipohitimu darasa la saba," anasema Zuberi.
Mjomba wa Zuberi, twaha yusuf Ugama anasema baada ya mpwa wake kumaliza darasa ya saba alichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kwale ndipo tatizo hilo liliporudi kwa kasi kubwa.
"Mwanzoni mwa 2011kabla ya kuanza kidato cha kwanza, tatizo lilirudi upya alipopelekwa Kizingani walimwandikia aende hospitali ya Rufaa Bombo iliyopo Tanga mjini. Pale alipewa huduma ya kupunguza maji na kupewa rufaa ya Muhimbili. Aliletwa jijini kwa matibabu," anasema Twaha.
Anasema tatizo hilo lilianza kuwa sugu na iliwalazimu kuhudhuria kliniki. "Tukiwa Muhimbili tulipatiwa huduma ya kliniki ilikuwa na ugumu kidogo kutokana na mgonjwa kutokuwa na kadi ya matibabu. Ilipofika Septemba 2012 daktari bingwa wa Moyo aliyekuwa akimhudumia alituambia kwamba hali ya mgonjwa itakuwa ngumu kutibika," anasema twaha.
Anasema Zuberi alisikia kauli ya daktari iliyomfanya akate tamaa ya kuishi "Alirudi Tanga na muda mfupi baadaye alizidiwa tena.
Ndipo mmoja wa wanafamilia alikutana na tabibu ambaye anatokea Tanga,anaitwa samwel shita ambaye yuko masomoni ya udaktar kwa sasa,aliamua kuchukua jukumu la kumsaidia uchunguzi upya,akisaidiana na daktari bingwa wa moyo dokta henry mayala katika hospital ya Sanitas .
Waligundua anatatizo la valve za moyo wake hivyo moyo kushindwa kufanya kazi vizur dokta mayala aliandika maelezo yakina na sababu za tatizo la zuberi kiundani nzaidi,Alieleza kutokana na tiba hiyo haipo hapa nchini ,inahitajika kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kubadili valve zake.
Baada ya hapo alifanyiwa tena uchunguzi katika hospitali ya regency,baaada ya uchunguz na matibabau sehemu hizi mbili,regency na sanitas ndipo matumini mapya yalirud kwa zuberi. Akiwa Regency Zuberi alifanyiwa vipimo na madaktari
Twaha anasema kiasi hicho cha fedha kitasaidia matibabu ya Zuberi yanayogharimu kiasi cha dola 2500 sawa na milioni 4 pamoja na fedha zingine kwa ajili ya tiketi ya ndege yeye na msindikizaji wake kwenda na kurudi pamoja na gharama nyingine watakapokuwa huko kwa matibabu.
Hospitali alizowahi kutibiwa
Kizingani iliyopo Kwale Tanga
Hospitali ya rufaa Bombo Tanga mjini
Hospitali ya taifa ya Muhimbili
Sandarya Medics Dar
Sanitaz Hospital Dar
Temeke Hospitali
Hospitali ya Regency