Baadhi ya Vijana waliopata mafunzo ya jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakionyesha jinsi ya kutengeneza mkaa huo wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.
Mmoja wa wahitimu akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.Kushoto ni Meneja Miradi wa Plan Wilayani Ilala Bw.Daniel Kalimbiya.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi akimsikiliza mmoja wa Vijana waliopata mafunzo ya jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi akiangalia mkaa mbadala wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.
Vijana waliopata mafunzo ya jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakimsikiliza Mgeni Rasmi wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.(Picha na Demetrius Njimbwi-Jeshi la Polisi).
=============== ========= ==============
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Vijana nchini wameshauriwa kuacha kubweteka na kuonekana mzigo kwa familia na badala yake wajikite katika ujasiriamali ili kupambana na hali ngumu ya maisha hatua itakayo wasaidia kuongeza kipato na kuinua uchumi wao.
Wito huo umetolewa mapema jana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya ujasiriamali wa kutengeneza mkaa unaotokana na mabaki ya takataka za majumbani na viwandani kwa Vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni yaliyofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Plan na kuendeshwa na Wakufunzi kutoka Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo (SIDO).
Mh. Mushi amesema kuwa, moja ya changamoto zinazowakabili vijana wengi ni kutokupenda kujishughulisha na badala yake hutumia muda wao mwingi katika kufanya mambo yasiyo na faida hali ambayo imekuwa ikichangia kurudisha nyuma jitihada zao za kujiletea maendeleo.
Alisema kuwa pamoja na mafunzo yaliyotolewa kwa vijana hao, bado wanajukumu la kutambua maendeleo yanaletwa na wao wenyewe kwa kuutumia ipasavyo ujuzi walioupata hatua itakayo saidia kufungua fursa ya ajira.
Aidha aliwataka vijana kuzingatia maadili ikiwa pamoja na kuthamini mafunzo waliyoyapata na kuwa na tabia ya kushirikiana katika mambo yatakayo wasaidia kuongeza ujuzi pamoja na kutanua wigo wa kibiashara.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa Shirika Plan Wilayani Ilala Bw. Daniel Kalimbiya amesema kuwa, bado wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuboresha maisha ya Watanzania ikiwa pamoja na kuwataka vijana kutokujiingiza katika vitendo viovu vya uhalifu ikiwemo kujiuza katika madanguro kwa kisingizio cha kukosa ajira.
“Tumieni fursa vyema mliyoipata hapa ili mjiletee maendeleo na sisi tutaendelea kushirikiana na kuviwezesha vikundi vya Vijana ambavyo vimekuwa vikifanya vizuri katika kujiletea maendeleo kwani malengo ya shirika letu ni kutetea haki za Watoto na Vijana”Alisema Kalimbiya
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Dar Es Salaam Hamwel Meena aliahidi kuwapatia vijana hao mikopo itakayowawezesha kununua mashine zitakazowawezesha kufanya kazi ya kutengeneza Mkaa mbadala kwa ufanisi ili kuokoa mazingira na kuufanya mji kuwa msafi kwakuwa mkaa huo unatengenezwa kutokana na takataka.