Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Nancy Sumari: Nililipwa Mshahara wa 120,000 Kwa Mwezi

$
0
0
Katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango wiki hii alifanya mahojiano na Miss Tanzania na Miss World Africa 2005, Nancy Sumari kuhusu mambo mbalimbali yanayomhusu katika maisha ya kabla na baada ya kutwaa mataji hayo makubwa na kuingia katika historia kama Miss Tanzania aliefanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya ulimbwende duniani.

Nancy ambaye hivi karibuni amezindua kitabu cha watoto alichokipa jina la Nyota Yako alielezea nini hasa kilichomsukuma hadi kuamua kuandika kitabu hicho na kusema ilitokana na baada ya kuwa mama na kujikuta kila akienda maduka ya vitabu anakosa vitabu vya watoto vilivyoandikwa na waandishi wa Tanzania na kukuta vingi ni kutoka nje ya nchi, hivyo kuamua kuandika kitabu ambacho watoto wa kike wa Tanzania wataweza kukisoma na kuvutiwa kufanya kile ambacho muandishi amekielezea. “Kwa hivi sasa kitabu kinapatikana maduka ya Scholastica Mlinani City na pia Novel Idea Masaki na Ohio kwa shilingi 5,000 tu” alisema Nancy.

Lakini Nancy alikuwa na stori ya kusisimua kwani anasema kabla ya kuingia kwenye mashindano ya urembo alilazimika kufanya kazi kama muuzaji katika duka la fenicha kwa mshahara wa shilingi lakini moja na ishirini kwa mwezi. Hii ilitokana na kukwama kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitivo cha Sheria kutokana na chuo hicho kutoruhusu mwanafunzi aliemaliza kidato cha nne kwa elimu ya Kenya kujiunga moja kwa moja kwa ajili ya shahada.

Nancy amesema alifanya kazi hiyo kwa moyo wote hadi alipopata nafasi ya kushiriki taji la Miss Dar Indian Ocean baada ya kuonwa na wandaaji wa shindano hilo na kuibuka mshindi wa pili na baadae kuibuka Miss Kinondoni na hatimaye Miss Tanzania huku akisema kufanya kila kitu bila kuogopa kushindwa ndio siri hasa ya kufanikiwa licha ya kutokuwa na uzoefu wowote katika suala la urembo wa wakati huo na kusema hatimaye alifanikiwa kupata nafasi ya kuingia chuo kikuu cha Dar es salaam na atatarajia kumaliza masomo yake mwezi Julai.

Alipoulizwa nini ushauri wake kwa vijana wanaochipukia alisema “Let’s all try to become better people, everyone makes mistake no one is perfect lakini ni muhimu kama binadamu kujitahidi kufanya vitu sahihi sawa na unapoona ua linafifia linamwagilizie maji likue na unapomuona mwenzio anahitaji msaada na unayo nafasi ya kumsaidia usisite”

Mahojiano yote yanapatikana katika:


Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akimsikiliza Nancy Sumari
Nancy Sumari akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Fina Mango

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>