Kwa siku nzima ya leo, mawasiliano ya mtandao katika nchi za Afrika Mashariki yamepatwa na kwikwi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni matatizo ya kiufundi yaliyoikumba mitambo ya kampuni ya Seacom, inayotoa huduma hiyo kwa njia ya mkongo upitao chini ya bahari.
Tayari Seacom, kupitia mtandao wake, imeomba radhi kwa kwikwi hiyo iliyosababisha tafrani kila mahali, ikiwemo Tanzania, na kuahidi kuirekebisha haraka iwezekanavyo.
Globu ya Jamii inaomba Kunradhi wadau kwa kukumbwa pia na kwikwi hiyo ambayo iko nje ya uwezo wetu. Tunaahidi kundeleza Libeneke mara tu mambo yatapotegamaa.
Kwa kuwa hii si kwikwi ya kwanza, tungependa kujua endapo kama hatua mbadala za makusudi zimewekwa ama zipo kukabiriana na kwikwi kama hii, ambayo kwa kweli inatoa raha kwa kukosesha wadau mawasiliano haya muhimu.
ANKAL